Kwa mujibu wa ripoti ya kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, Hujjatul-Islam wal-Muslimin Arif Hussein Waahidi, Makamu wa Rais wa Baraza la Wanazuoni wa Kishia Pakistan, alihudhuria na kutoa hotuba katika mkutano unao fanyika kila mwaka wa hija ulio andaliwa na Baraza la Wanazuoni wa Pakistan huko Islamabad, Pakistan.
Katika hotuba yake iliyokuwa na anuani isemayo "Falsafa na Utukufu wa Hija", alilitaja hija kuwa ni alama ya umoja wa Umma wa Kiislamu wote duniani, na akasisitiza umuhimu wa kunufaika na fursa hii adhimu kwa ajili ya kuimarisha mshikamano wa Waislamu.
Hujjatul-Islam wal-Muslimin Arif Waahidi, akizungumzia baadhi ya matatizo na changamoto zinazowakabili mahujaji, alitoa wito maalum kwa viongozi ili waweze kutatua matatizo haya, na akasisitiza juu ya haja ya kuandaa mazingira bora zaidi kwa ajili ya ustawi na faraja kwa mahujaji.
Maoni yako